SIMBA YAVUTA KASI KITAIFA NA KIMATAIFA, MANDALIZI KUANZA

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa wiki ijayo wanatarajia kuingia kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za ushindani kitaifa na kimataifa kwa msimu wa 2024/25.

Mchezo uliopita Simba ilivuna pointi tatu dhidi ya Dodoma Jiji ulichezwa Uwanja wa KMC, Complex ilikuwa Machi 14 2025 baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 6-0 Dodoma Jiji.

Kwenye mchezo huo kiungo mshambuliaji Kibu Dennis alifungua akaunti ya mabao kwa kufunga mabao mawili na pasi mbili hivyo alihusika kwenye mabao manne katika mchezo huo alipachaguliwa kuwa mchezaji bora.

Ikumbukwe kwamba mara ya mwisho Kibu kufunga ndani ya ligi ilikuwa Novemba 5 2023 kwenye Kariakoo Dabi na Novemba 5 2024 alitimiza mwaka mmoja bila kufunga katika mechi za ligi licha ya kuwa ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu, Fadlu Davids.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa wanatambua mechi zilizopo hivyo wataanza kufanya maandalizi wiki ijayo.

“Maandalizi hatujaanza kwa sasa wachezaji wameruhusiwa wapo kwenye mapumziko, wapo waliopo kwenye timu zao za taifa, Tanzania Uganda, Guinea hivyo bado hatujaanza kila mmoja ameenda kuipigania timu yake.

“Tunategemea wiki ijayo kurejea uwanja wa mazoezi ambapo tutaanza maandalizi kwa ajili ya mchezo wa CRDB Federation Cup dhidi ya Big Man Machi 27 2025.

“Baada ya hapo tunatarajia kuondoka muda wowote kuanzia Machi 28 kwenda Misri jwa ajili ya mchezo wetu wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Al Masry.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.