CHADRACK Boka beki wa kikosi cha Yanga ambao ni vinara wa ligi amebainisha kuwa ligi ya Tanzania ni ngumu jambo ambalo linawafanya wazidi kupambana kupata matokeo kwenye mechi ambazo wanacheza.
Boka ndani ya ligi kafunga bao moja ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Pamba Jiji uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba katika mchezo huo alipachika bao hilo kwa pigo huru akiwa nje ya 18.
Baada ya dakika 90, Februari 28 ubao ulisoma Pamba Jiji 0-3 Yanga wakisepa na pointi tatu mazima ugenini, ni mabao 58 Yanga imefunga kibindoni ikiwa nit imu yenye mabao mengi katika ligi namba nne kwa ubora.
Beki huyo amebainisha kuwa kila mechi kwao wanaichukulia kwa uzito mkubwa hiyo inatokana na ugumu uliopo katika mechi zote za ligi ambazo wanacheza.
“Kila mchezo kwetu tunauchukulia kwa uzito mkubwa kwa kuwa hakuna mechi rahisi na ligi ni ngumu hilo lipo wazi. Tunaangalia zaidi mechi zetu zote kikubwa ambacho tunahitaji ni kupata matokeo mazuri.”
Kuna mastaa wawili ambao ni vinara wa utupiaji ndani ya kikosi cha Yanga ambao ni Prince Dube na Clement Mzize hawa wote kila mmoja katupia mabao 10.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.