KUNA mgawanyo wa vita ya pande nne kwa sasa ile ya kwanza ni ya ubingwa kwa timu zilizo ndani ya tano bora kinara akiwa ni Yanga mwenye pointi 58 anafuatiwa na Simba pointi 57 hizi mbili zimecheza mechi 22 kila mmoja.
Azam FC nafasi ya tatu kwenye msimamo pointi 48, Singida Black Stars nafasi ya nne pointi 44 na Tabora United nafasi ya tano kibindoni pointi zake 37.
Daraja la tatu ni timu zinazopambania kumaliza ndani ya 10 bora zikiongozwa na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 6 ikiwa na pointi 30 huku safu yao ya ushambuliaji baada ya mechi 23 ikiwa imeruhusu mabao 18.
Kipande kigumu ni zile timu ambazo zinapambana kujinasua kwenye mstari mwekundu wa kushuka daraja ambapo ni lazima timu mbili zitashuka mazima na mbili zitacheza mchezo wa playoff.
Ken Gold ngoma nzito kwenye msimamo wa ligi baada ya mechi 23 inaburuza mkia ikiwa na pointi zake kibindoni 16 haijawa na mwendo mzuri ikiwa ni msimu wake wa kwanza.
Ni ushindi kwenye mechi tatu, sare katika mechi 7 na imepoteza jumla ya mechi 13 ikiwa ni timu iliyofungwa mabao 40 na safu ya ushambuliaji imetupia mabao 20.
Ndani ya dakika 2,070 timu hiyo ina wastani wakufungwa kila baada ya dakika 51 na safu ya ushambuliaji ina wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 103.
Namba mbili ni Tanzania Prisons nayo ipo kwenye mstari mwekundu ina pointi 18 ikiwa nafasi ya 15 ushindi ni kwenye mechi nne, sare sit ana kichapo kwenye mechi 13.
Daraja la nne ni mbili ambazo zinapambana kuondoka kwenye eneo la kucheza Play Off ambapo ni Kagera Sugar na Pamba kwa sasa zipo kwenye mstari huo.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.