KARIAKOO DABI KITAWAKA LEO

MACHI 18 2025 kutakuwa na kazi kwa wababe wawili kwenye Kariakoo Dabi ya Wanawake Uwanja wa KMC, Complex kwa wababe wawili Simba Queens dhidi ya Yanga Yanga Princess kukutana uwanjani kwenye msako wa pointi tatu ndani ya dakika 90 za kazikazi.

Ikumbukwe kwamba Simba Queens ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 34 baada ya mechi 12 ambapo ndani ya dakika 1,080 safu yao ya ushambuliaji imekusanya jumla ya mabao 43 ikiwa na wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 25.

Na kibindoni wamekusanya pointi 34 wanashikilia rekodi yakucheza mechi zote bila kupoteza hivyo kazi nyingine mbele ya mtani wake wa jadi itakuwa ni kulinda rekodi hiyo huku Yanga wakipambana kutibua rekodi yao.

  Yanga Princess kwenye msimamo ipo nafasi ya tatu na pointi 21 baada ya mechi 11 ni dakika 990 imeshuka uwanjani safu ya ushambuliaji imetupia mabao 21 ikiwa na wastani wakufunga bao moja kila baada ya dakika 47 ni mechi mbili ilipoteza.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga Princess amesema kuwa wapo tayari kwa mchezo wa ligi na maandalizi yapo vizuri kutokana na timu hiyo kutoka kutwaa taji la Samia Cup hivyo mwendelezo wa kupata ushindi bado upo kwa wachezaji.

“Ni timu ambayo imetoka kuchukua taji la Samia Cup hivyo hii inafanya maandalizi mazuri kuendelea kuwa kwenye mwendo huo kikubwa tupo tayari na kila upande umetimiza majukumu yake kwa umakini.”

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba Queens amesema kuwa wamefanya maandalizi mazuri kwa ajili ya mchezo huo ambao wanaamini utakuwa na ushindani mkubwa.

“Tumefanya maandalizi mazuri na tulianza baadaya kutoka Arusha hivyo kikubwa ni utayari na wachezaji wanatambua umuhimu wa mchezo wetu huu, mashabiki tujitokeze kwa wingi.”

Mchezo huu unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC Complex saa 10 jioni kwa wababe hawa kuwa kazini kusaka pointi tatu muhimu.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM. Kuna kazi mpya inaandaliwa inaitwa Moyo Wangu Unavuja Damu usipange kukosa.