HUSSNA AFICHUA MAZITO ALIYOKUTANA NAYO OMAN ALIPOISHI MIAKA 2 – AFIKA na WADADA WENGINE 6 AIRPORT…

Watanzania 7 waliokuwa wakifanya kazi za ndani nchini Oman wamerejea nchini ambapo @zali_mapito aliwapokea na kuzungumza nao kuhusu maisha waliyopitia wakiwa nchini Oman na sababu zilizowarejesha nchini.

Miongoni mwao yupo mwanadada Husna, ambaye amefanya kazi Oman kwa miaka 2, akiwa tayari ameshapitia kwenye nyumba za mabosi wake watatu.

Husna ameeleza yote kuhusu kubadilisha mabosi hao kwa miaka miwili, akitaja sababu za kiafya na zinginezo zilizochangia.

Pia, Husna ametoa ushauri kwa wadada wengine wanaoendelea kufanya kazi nje ya nchi.