KIUNGO WA KAZI ANASEPA YANGA

INATAJWA kuwa kiungo wa kazi ndani ya kikosi cha Yanga huenda akasepa baada ya msimu wa 2024/25 kugota mwisho kwa kuwa amepata timu ambayo inahitaji huduma yake kutokana na uwezo alionao.

Ni Aziz Ki ambaye ni chaguo la kwanza la Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi kwenye eneo la kiungo akiwa ni mkali kwenye mapigo huru hasa penati na faulo ambapo kwa msimu huu Yanga ikiwa imepata penati 7 yeye alipewa jukumu kupiga sita.

Katika penati hizo ni nne alipata na mbili makipa waliokoa hatari hizo ilikuwa kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar Uwanja wa KMC Complex na Tabora United uliochezwa Uwanja wa Azam Complex.

Taarifa zinaeleza kuwa kuna timu moja kutoka Libya ambayo imefanya mawasiliano kwa ukaribu na mabosi wa Yanga na nyingine ni Kaizer Chiefs ambayo ilikuwa inahitaji saini ya kiungo huyo kwa muda mrefu.

Uwezekano ni mkubwa kwa nyota huyo mwenye mabao 7 ndani ya ligi na pasi sita kusepa ndani ya Bongo kwa ajili ya kupata changamoto mpya katika ligi nyingine nje ya ardhi ya Tanzania.

Hivi karibuni Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa kumekuwa na timu nyingi ambazo zinahitaji wachezaji kutoka Yanga hilo linatokana na ubora uliopo kwa wachezaji hao.

“Kuna timu nyingi ambazo zinahitaji huduma kutoka kwa wachezaji wetu hizo taarifa tunazitambua na wapo ambao wamekuja mezani kuleta ofa tunajua, tutatoa taarifa baada ya msimu kuisha kwa sasa malengo yetu ni kuona kwamba tunatwaa ubingwa wa ligi.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.