HAMISA MOBETTO ALIPUKA: “NIMECHOKA, NAOMBENI MNIACHE!”

Mwanamitindo na mjasiriamali maarufu, Hamisa Mobetto, ambaye pia ni mke wa nyota wa klabu ya Yanga SC na raia wa Burkina Faso, Stephanie Aziz Ki, amefunguka kwa uchungu kupitia ‘insta stories’ baada ya kuchoshwa na maneno ya watu mitandaoni.

Kupitia ujumbe aliouchapisha, Hamisa ameonyesha kuchoka na mashambulizi ya mara kwa mara kutoka kwa watumiaji wa mitandao ya kijamii.

“Samahani sana, mie si jalala lenu jamani! Kila siku mkipata takataka mnakuja kunitupia. Naombeni tu mniache, nimechoka sana.

Najionea tabu tupu kila siku kuandamwa, sijui niliwakosea wapi,” aliandika Hamisa Mobetto.

Kauli yake inakuja baada ya kuandamwa kwa siku mbili mfululizo kufuatia mzozo unaomhusisha aliyekuwa rafiki yake, Rushaynah, ambaye ni mke wa zamani wa Haji Manara.

Rushaynah amekuwa akidaiwa kumzungumzia mume wa Hamisa, Aziz Ki, hali iliyochochea gumzo mitandaoni.