DUBE NA MILOUD WAMEKIMBIZA KWA FEBRUARI

MSHAMBULIAJI wa Yanga, Prince Dube na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi wamekimbiza ndani ya Februari kwa kusepa na tuzo kutoka Ligi Kuu Bara wote wakiwa wanatokea Jangwani.

Ndani ya Februari kwenye mechi tano rekodi zinaonyesha kuwa Dube alihusika kwenye mabao matano na alifunga matano hivyo akahisika mojamoja kwenye mchango wa mabao 10.

Ni mechi 7 alicheza Dube akikomba dakika 562 huku kocha Miloud Hamdi kwenye mechi 5 ambazo alikuwa kwenye bechi ushindi katika mechi 4 sare ilikuwa moja na alishuhudia safu ya ushambuliaji ikitupia jumla ya mabao 16.

Hamdi alimshinda Fadlu Davids wa Simba na Fred Minziro wa Pamba ambao aliingia nao fainali huku kwa Dube akimshinda Aziz Ki wa Yanga na Seleman Bwenzi wa Ken Gold.

Dube ni chaguo la kwanza la Miloud ambapo kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup dhidi ya Coastal Union ya Tanga alianza kikosi cha kwanza.

Baada ya dakika 90 ubao wa Uwaja wa KMC Complex Machi 12 ulisoma Yanga 3-1 Coastal Union ambapo mabao mawili yalifungwa na Maxi Nzengeli na bao moja lilifungwa na Clement Mzize.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.