YANGA leo Machi 12, 2025 itakutana na Coastal Union katika hatua ya 32 bora ya Kombe la Shirikisho la CRDB. Mchezo huu utachezwa saa 10:00 jioni katika Uwanja wa KMC Complex jini Dar.
Yanga SC, mabingwa watetezi wa michuano hii, wanatarajia kuendeleza rekodi yao nzuri dhidi ya Coastal Union. Katika rekodi za nyuma, timu hizi zimekutana mara 23, ambapo Yanga imeshinda mechi 15, Coastal Union imeshinda mechi 3, na mechi 5 ziliisha kwa sare.
Mara ya mwisho timu hizi zilipokutana katika fainali ya Kombe la Shirikisho mwaka 2022, mchezo uliisha kwa sare ya 3-3 baada ya dakika 120, na Yanga ikashinda kwa penalti 4-1.
Mshindi wa mechi ya leo ataingia hatua ya 16 bora ya michuano hii.