UWANJA WA MKAPA WAFUNGIWA, SIMBA HATIHATI KUCHEZA KIMATAIFA

SHIRIKISHO la Mpira wa Miguu Afrika, (CAF) limeufungia Uwanja wa Benjamin Mkapa kwa muda kutokana na eneo la kuchezea kuendelea kupungua ubora wake hivyo kuna hatihati ikiwa maboresho hayatakamilika mapema wawakilishi wa Tanzania kwenye anga la kimataifa Simba kutoutumia uwanja huo.

Taarifa iliyotolewa na TFF imeeleza kuwa CAF imeelekeza eneo hilo liboreshwe haraka kufikia viwango vinavyotakiwa ili kuepeuka uwanja huo kufungiwa kwa muda mrefu.

Mechi ya robo fainali ya Kombe la Shirikisho CAF kati ya Simba v Al Masry imepangiwa kuchezwa uwanja huo Aprili 9 2025 ili kuondoa usumbufu Shirikisho la Mpira Tanzania, (TFF) limetakiwa kutuma jina la uwanja mbadala utakaotumiwa na Simba Machi 14 2025.

Taarifa hiyo imebainisha kuwa CAF itafanya ukaguzi wa Uwanja wa Mkapa, Machi 20 2025 ili kuona maboresho ambayo yamefanyika kabla ya kuamua kuuruhusu utumike ama ufungiwe.

Ikumbukwe kwamba mbali na mashindano ya kimataifa ya CAF uwanja huo umepangwa kutumika kwa ajili ya mashindano ya CHAN Agosti 2025.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.