Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Cde Gerson Msigwa amesema uwanja wa Mkapa uko tayari kwa ukaguzi wa CAF hata leo au kesho wala sio tarehe 20 March, 2025, waliosema wao.
Msigwa akizungumza na Bin Kazumari amesema ameshangaa kuona CAF wanasema kiwanja kibovu na kimefungiwa kwa muda ilihali kiwanja kiko sawa bin sawia na kiko tayari kwa ukaguzi, eneo la kuchezea liko vizuri sana kama linavyoonekana kwenye picha mnato na mjongeo ambazo Bin Kazumari amepewa na Katibu Mkuu wa Wizara.