Timu ya Manchester United rasmi sasa imetangaza kujenga Uwanja mpya utakaoingiza watazamaji 100,000 kwa wakati mmoja.
Uwanja huo ndio utakuwa Uwanja mkubwa zaidi katika Taifa la Uingereza kwani Wembley ndio Uwanja mkubwa kwa sasa na unachukua watu 90,000.
Ukubwa wa Uwanja huu utakuwa sawa na Uwanja kama Uwanja wa Barcelona Camp Nou.
Taarifa hiyo imetolewa rasmi na klabu hiyo lakini pia itakuwa sehemu ya Utalii maana utakuwa Uwanja wa Kisasa Zaidi England.