HASIRA ZA SIMBA KUHAMIA HAPA KISA KARIAKOO DABI

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa hasira zakukosa mchezo wa Kariakoo Dabi ambao ulitarajiwa kuchezwa Machi 8 2025 Uwanja wa Mkapa watazihamishia kwa wapinzani wao TMA Stars mchezo wa CRDB Federation Cup.

Ikumbukwe kwamba mchezo huo ulikuwa ukisubiriwa kwa shauku kubwa kati ya Yanga na Simba, Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) ilitoa taarifa kwamba utangiwa siku nyingine kutokana na Simba kutoa malalamiko kuwa walinyimwa haki ya kutimiza kanuni ya kufanya mazoezi kwenye uwanja siku moja kabla ya mchezo.

Ahmed Ally, Meneja wa Idara ya Habari Simba amesema kuwa walifanya maandalizi makubwa kwa ajili ya mchezo wao wa Machi 8 lakini ilishindikana hivyo hasira zote watazihamishia kwenye mchezo wao dhidi ya TMA Stars.

“Tulifanya maandalizi makubwa kwa ajili ya mchezo wetu wa Machi 8 ambao uliahirishwa sasa nguvu zetu ni kwenye mchezo wetu dhidi ya TMA tunahasira vibaya kwa kuwa tulifanya maandalizi makubwa, tunawaheshimu wapinzani wetu na tupo tayari kwa mchezo.”

Simba itawakaribisha TMA Stars kwenye mchezo wa CRDB Federation Cup, Uwanja wa KMC Complex saa 10:00 jioni.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.