CHAMA CHA SOKA CHA VILABU AFRIKA [ACA] KIMESAINI MKATABA WA USHIRIKIANO NA CAF

Rasmi leo Chama Cha Soka cha vilabu Afrika [ACA] chini ya Mwenyekiti wake Eng. Hersi Said kimesaini Mkataba wa ushirikiano na Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika [CAF].

Hafla hii imefanyika kwenye mji wa Cairo, Misri na kuhudhuriwa na Viongozi wa juu wa Taasisi hizi mbili, Eng Hersi na Rais wa CAF, Dkt. Patrice Motsepe.