AHMED Arajiga ametangazwa kuwa mwamuzi wa kati wa mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 8 2025 ambapo wababe wawili wanatarajiwa kukutana Yanga na Simba.
Ikumbukwe kwamba Arajiga alikuwa mwamuzi kwenye mchezo wa Mzizima Dabi uliochezwa Uwanja wa Mkapa baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Azam FC wababe hao walipogawana pointi mojamoja baada ya mchezo kukamilika.
Ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza ni Ramadhan Kayoko alikuwa ni mwamuzi wa kati ila mzunguko wa pili jina lake halipo kwenye orodha ya waamuzi. Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao wa Uwanja wa Mkapa ulisoma Simba 0-1 Yanga, bao la Kelvin Kijili aliyejifunga lilidumu mpaka mwisho wa mchezo.
Karim Boimanda Ofisa Habari wa Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB) amesema kuwa kwenye asilimia ya maandalizi wapo juu sana kutokana na kila kitu kuwa kwenye mpangilio mzuri huku akiwataja watakaosimamia mchezo huo.
Salim Singano, Mohamed Mkono, (mwamuzi msaidizi namba moja) hawa kutoka Tanga Kassim Mpanga, (mwamuzi msaidizi namba mbili) kutoka Dar, Amina Kyando,(mwamuzi wa akiba) kutoka Morogoro, Soud Abdi kutoka Dar ikiwa ni baadhi ya maofisa kwenye mchezo huo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa mwamuzi wa kati atakuwa Ahmed Arajiga.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.