TABORA UNITED KUTUMIA CCM KIRUMBA

Timu ya Tabora United itatumia Uwanja wa CCM Kirumba uliopo jijini Mwanza kama Uwanja wa wake wa nyumbani katika mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya JKT Tanzania, utakaochezwa siku ya ljumaa Machi 07 saa 10:00 jioni.

Tabora United FC itatumia Uwanja huo kutokana na kufungiwa kwa Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi ambao ulikuwa ukitumika kwa michezo yao ya nyumbani.

Taarifa ya klabu hiyo iliyotolea leo mchana imewatoa hofu mashabiki wa klabu hiyo kwa kueleza, uongozi wa Tabora United kwa serikali ya mkoa pamoja na wadau mbalimbli unaendelea na ukarabati wa Uwanja Ali Hassan Mwinyi ili uweze kutumika kwenye michezo ya ligi kuu iliyosalia.