ERASTO Nyoni kiraka anayetimiza majukumu yake ndani ya kikosi cha Namungo kinachonolewa na Kocha Mkuu, Juma Mgunda ameweka wazi kuwa nyota Clatous Chama amebadilika hasa kwenye upande wa spidi ila watu wanamtazama kwa mazoea.
Ipo wazi kwamba Chama ni mchezaji wa kwanza kutambulishwa ndani ya kikosi cha Yanga kwenye dirisha kubwa la usajili ilikuwa ni Julai Mosi 2024 ambapo aliibuka hapo akiwa ni mchezaji huru baada ya kumaliza kandarasi yake ndani ya kikosi cha Simba.
Chama alipokuwa Simba alikuwa chaguo la kwanza lakini kwa sasa ndani ya kikosi cha Yanga ambacho kwenye anga la kimataifa kimegotea hatua ya makundi sio chaguo la kwanza amekuwa akipokezana namba na Aziz Ki ambaye naye ni kiungo mshambuliaji wakati mwingine Pacome.
Nyoni aliwahi kucheza na Chama katika kikosi cha Simba kabla ya kukutana na Thank You na sasa anaendelea kutimiza majukumu ndani ya Namungo ambayo Februari 27 2025 ilishuhudia ubao wa Uwanja wa Azam Complex ukisoma Azam FC 1-1 Namungo.
Kiungo huyo amesema: “Chama amebadilika kwenye suala zima la uchezaji ila kwa kuwa yupo kwenye timu mpya watu wanamuangalia kwa mazoea tu ninaweza kusema hivyo. Ukimuangalia kwenye uchezaji wake ameongezeka spidi lakini kuna watu hawawezi kujua.
“Ninaweza kusema ni kumzoea si unamuona namna anavyocheza. Watu wamemzoea Chama lakini hawataki kumuona anachezaji kule kuna wachezaji ambao ni wazuri hivyo ushindani utakuwa mkubwa, lakini hapana amebadilika uchezaji mwangalie kwenye mechi zote amebadilika amekuwa kwenye spidi.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.