NYOTA Steven Mukwala mshambuliaji wa Simba amesema kuwa kazi kubwa ni kupambana kwenye mech izote kupata matokeo mazuri kutokana na ushirikiano ambao upo kwenye timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Kwenye msimamo wa ligi Simba ni namba mbili baada ya mechi 21 imekusanya jumla ya pointi 54 vinara wakiwa ni Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Miloud Hamdi.
Simba mchezo wao uliopita wa ligi baada ya dakika 90 ubao ulisoma Coastal Union 0-3 Simba mtupiaji wa mabao yote akiwa ni Mukwala akisepa na tuzo ya mchezaji bora na mpira wake baada ya kufunga hhat trick.
Ni mabao 8 anafikisha Mukwala ndani ya ligi akiwa namba mbili wa wakali wakucheka na nyavu ndani ya kikosi cha Simba ni Jean Ahoua mwenye mabao 10 huyu ni namba moja, Mukwala na Leonal Ateba wote wametupia mabao 8.
Mukwala amesema kuwa kikubwa ambacho wanapambana ni kupata matokeo mazuri na wanaamini kazi itakuwa kubwa kwenye mechi zinazofuata.
“Shukrani kwa mashabiki ambao wapo nasi bega kwa bega kutokana uwepo wao kwenye mechi zetu zote, ambacho tunapambana ni kupata matokeo mazuri tunaamini itakuwa hivyo kwenye mechi zetu zote.”
Kituo kinachofuata kwa Simba ni Kariakoo Dabi dhidi ya Yanga mchezo unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Machi 8 2025.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.