AHMED Ally, Meneja wa Idara ya Habari na Mawasiliano Simba amesema kuwa kupata sare mbele ya Azam FC kwa kuvuna pointi moja haikuwa rahisi kutokana na ubora wa mpinzani wao na kuna mechi 10 ambazo zimebaki hizo ni za machozi na damu kutokana na kila timu kupambana kuvuna pointi tatu muhimu.