MASHUJAA YAMFUTA KAZI KOCHA MKUU MOHAMED ABDALLAH ‘BARESS’

Klabu ya Mashujaa Fc imethibitisha kumfuta kazi kocha mkuu Mohamed Abdallah ‘Baress’ baada ya kufikia makubaliano ya kuvunja mkataba na kocha huyo kufuatia mwenendo usioridhisha wa klabu hiyo vikiwemo vipigo viwili mfululizo dhidi ya Yanga Sc (5-0) na Singida Black Stars (3-0)

Taarifa ya Februari 26 iliyotolewa na klabu hiyo imeeleza kuwa Uongozi wa klabu hiyo umesitisha mkataba wa kocha wa viungo Hussein Bunu pamoja na kocha wa makipa Rafael Nyendi.

Kwa sasa timu itakuwa chini ya kocha msaidizi Charles Fredie wakati mchakato wa haraka wa kumpata kocha mkuu ukiendelea.

“Uongozi wa Klabu unapenda kuwashukuru makocha hao kwa mchango wao ndani ya Klabu yetu na unawatakia kila la kheri katika majukumu yao mapya.”—imesema sehemu ya taarifa hiyo