HUYU HAPA ALIHUSIKA KUWANYIMA USHINDI SIMBA MZIZIMA

PASCAL Msindo kwa asilimia 80 aliwanyima ushindi Simba katika mchezo wa Ligi Kuu Bara Februari 24 2025 kwenye Mzizima Dabi kutokana na kutimiza majukumu yake kwa umakini asilimia 100.

Utulivu kwenye miguu yake ulikuwa ukiwavuruga mabeki wote wa Simba ambao ni watengeneza mipango namba moja kwa kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Alikuwa anatokea katika matukio yote na hata wakati Mpanzu anakwenda kufunga bao la kusawazisha tayari alikuwa anakaribia kumkuta lakini spidi ya Mpanzu ikamkosesha namna kuzuia mpira ule.
Mwisho Simba 2-2 Azam FC, Zidane mchezaji bora wa mchezo akitumia pasi ya Feisal Salum kumtungua Camara.
Dakika ya 41 wakati Kapombe akiwa anaelekea ndani ya 18 na mpira kijana alislide na kucheza mpira alirudia tena dakika ya 56 akiwa kwenye ubora mkubwa na amekuwa akifanya hivyo kwenye mechi nyingi ndani ya Azam FC.
Mpole ukimuona, mcheshi kweli halafu mkorofi nje ya uwanja lakini ndani ya uwanja anapiga kazi kinomanoma. Kapombe ni imara kwenye mipira ya krosi akiwa nje ya 18 jambo ambalo lilikuwa likikwama kufanikiwa kwenye miguu ya kijana Msindo ambaye alipewa majukumu kwa ushirikiano na wachezaji wengine.

Mshindo akizungumza na Saleh Jembe ameweka wazi kuwa ulikuwa ni mchezo mgumu ambao kila timu ilikuwa na wachezaji bora na ambacho kilikuwa kinahitajika ni matokeo mazuri jambo lililowafanya wajitume mwanzo mwisho.

“Ulikuwa ni mchezo mgumu hasa ukizingatia kwamba timu zote ni bora hivyo kikubwa ambacho tulikuwa tunahitaji ni kuona kwamba tunapata matokeo mazuri, haikuwa kazi nyepesi lakini tunamshukuru Mungu kwa tulichokipata.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.