VINARA wa Ligi Kuu Bara ambayo ni namba nne kwa ubora Afrika, kasi yao imezidi kuwa kwenye kwenye eneo la ushambuliaji huku wakivuna pointi tatu nje ndani mbele ya Mashujaa na ndani ya dakika 180 wamevuna pointi sita msimu wa 2024/25.
Kwenye idadi ya mabao ya kufunga Yanga imezidi kuongeza hazina yake ikiwapoteza Simba kwenye kasi ya mabao ya kufunga ndani ya uwanja. Simba ni mabao 41 safu ya ushambuliaji ikitupia jumla ya mabao 41 baada ya kucheza mechi 19.
Yanga ni mabao 55 imefunga baada ya kucheza jumla ya mechi 21 ndani ya ligi na kinara wa utupiaji ni Clement Mzize akiwa na mabao 10 msimu wa 2024/25 akiwa na pasi nne za mabao.
Ikumbukwe kwamba Februari 23 2025 ubao wa Uwanja wa Lake Tanganyika ulisoma Mashujaa 0-5 Yanga ambapo pointi tatu zilirejea Jangwani.
Mabao ya Duke Abuya dakika 31, Prince Dube dakika ya 48, Khalid Aucho dakika ya 53 kiungo Clatous Chama alitupia mabao mawili ilikuwa dakika ya 74, 83 na mchezaji bora kwenye mchezo huo alichaguliwa Pacome.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.