BENCHI la ufundi la Simba limeweka wazi kuwa lipo tayari kwa mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Azam FC ambao ni Mzizima Dabi unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa, Februari 24 2025.
Simba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza walipata ushindi wa mabao 2-0 ubao ukifunguliwa na Leonel Ateba ambaye alifunga bao lake la kwanza ndani ya msimu na Fabrince Ngoma alipachika bao moja kwenye mchezo huo.
Wababe hao wanatarajiwa kusaka pointi tatu ndani ya uwanja mchezo ambao unatarajiwa kuchezwa saa 1:00 usiku ambapo awali ulitarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, sasa utachezwa Uwanja wa Mkapa.
Fadlu Davids, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wanatambua kwamba ushindani ni mkubwa na wataingia kwa tahadhari kusaka ushindi ndani ya uwanja.
“Kila mchezaji yupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu na tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu na ushindani ni mkubwa ambapo kila mmoja anahitaji kuona pointi tatu ndani ya uwanja.”
Lusajo Mwaikenda nyota wa Azam FC ameweka wazi kuwa wataingia kwa tahadhari kusaka pointi tatu muhimu kwa kuwa mchezo wa mzunguko wa kwanza walipoteza.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.