MKALI WA MABAO YA MBALI KUWAVAA SIMBA

KUELEKEA Mzizima Dabi mchezo unaotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa wababe hawa wawili kuna mkali wa mabao ya mbali yupo ndani ya kikosi cha Azam FC huenda akawapa tabu wapinzani wao wakikutana ndani ya dakika 90 za kuvuja jasho.

Ni Yoro Diaby nyota wa Azam FC anashikilia rekodi yakuwa nyota aliyefunga bao kwa umbali mrefu zaidi ilikuwa Februari 15 2025 dhidi ya Mashujaa akiwa nje kabisa ya 18 kwenye eneo la Azam FC.

Alipachika bao la pili wakati wakishinda mabao 2-0 kwa mguu wake wa kulia dakika ya 81, alimsoma kipa wa Mashujaa alikuwa ametoka kidogo na hiyo ni asili ya Camara kipa wa Simba hivyo Mzizima Dabi inazidi kuwa kwenye joto kali kwa sasa.

Camara ni kipa namba moja ndani ya kikosi cha Simba kwenye mechi 19 ambazo amecheza akikomba dakika 1,710 kashuhudia ukuta wa timu hiyo ukiruhusu mabao 6.

Kwenye mabao hayo sita ni mawili walijifunga wachezaji wa timu yake ilikuwa ni Kelvin Kijili dhidi ya Yanga kwenye Kariakoo Dabi na Ladack Chasambi kwenye mchezo wa ligi dhidi ya Fountain Gate.

Kazi kubwa inatarajiwa kuwa kwa wababe hao ambapo kila timu inahitaji ushindi ikumbukwe kwamba kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza baada ya dakika 90 ubao ulisoma Azam FC 0-2 Simba na pointi tatu zikawa mali ya mnyama.

Azam FC kwenye msimamo ni nafasi ya tatu huku safu ya ushambuliaji ikiwa imetupia mabao 29 inakutana na Simba ambayo safu ya ushambuliaji imetupia mabao 41.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.