MERIDIANBET YAZISHIKA MKONO TIMU 2 ZA MPIRA LEO

Katika kuendelea na juhudi zake za kusaidia maendeleo ya michezo nchini, kampuni ya Meridianbet leo imetoa msaada wa jezi kwa timu ya Rising Star FC na Kamili Gado. Msaada huu ni sehemu ya dhamira ya Meridianbet kuhamasisha na kukuza michezo, hasa soka, na kutoa fursa kwa wachezaji kuonyesha uwezo wao kwa ufanisi.

Timu ya Rising Star FC, inayojivunia vijana wenye talanta na ari kubwa ya kushinda, imepokea jezi mpya za kisasa zitakazowasaidia wachezaji kuonekana vizuri uwanjani. Vilevile, Kamili Gado, ambaye ni mfano wa mafanikio katika soka la Tanzania, amepokea msaada wa jezi ambazo atazitumia kwa mazoezi na mashindano ya kimataifa.

Kwa upande wa michezo Jumamosi ya leo, suka jamvi lako na Meridianbet huku ukikumbuka kucheza michezo ya Kasino ya mtandaoni kama vile, Poker, Roullette, Aviator, Wild Icy Fruits, Keno na mingine kibao.

Meridianbet, ikiwa ni sehemu ya jamii, imedhamiria kutoa mchango katika maendeleo ya michezo kupitia msaada huu, huku wakizingatia umuhimu wa kuwawezesha wachezaji kupata vifaa bora ili waweze kufikia malengo yao.

Mwakilishi wa Meridianbet Nancy Ingram alisema: “Tunajivunia kuwa sehemu ya mafanikio ya Rising Star FC na Kamili Gado. Tutaendelea kusaidia kukuza michezo na vipaji nchini, kwani ni sehemu ya dhima yetu ya kusaidia jamii katika sekta mbalimbali.”

Huu ni mchango muhimu kwa timu za vijana na wachezaji wanaojitolea kwa michezo, na Meridianbet itaendelea kuhakikisha inatoa msaada wa kijamii kwa maendeleo ya taifa letu kupitia michezo.

Vilevile timu hizo baada ya kupokea msaada huo waliishukuru sana Meridianbet na kusema kuwa msaada huo ni mwangaza kwa upande wao kwani mahitaji ni mengi sana hasa kwenye hizi timu ndogo ambazo bado zinajitafuta. Jisajili na ubashiri na meridianbet.