‘DERBY’ YA MZIZIMA KATI YA SIMBA DHIDI YA AZAM KUPIGWA JUMATATU KWA MKAPA

Mchezo wa ‘Derby’ ya Mzizima kati ya Simba Sc dhidi ya Azam utakayopigwa Jumatatu Februari 24, 2025 umehamishwa kutoka uwanja wa KMC Complex, Mwenge sasa utapigwa Katika uwanja wa Benjamin Mkapa, Chang’ombe

Taarifa ya leo Februari 22, 2025 iliyotolewa na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imeeleza kuwa mchezo huo utachezwa majira ya saa 1:00 usiku Februari 24, 2025 tofauti na saa 10:00 alasiri kama ilivyopangwa awali

Aidha, TPLB imebainisha sababu ya mabadiliko hayo kuwa ni kutoa nafasi kwa mashabiki wengi zaidi kuhudhuria mchezo huo ambao ni moja ya michezo mikubwa ya Ligi Kuu ya NBC inayovuta hisia za watu wengi.

Uwanja wa Benjamin Mkapa wenye uwezo wa kuingiza mashabiki 60,000 umekuwa ukitumika kwa michezo mingi mikubwa na inayohusisha mashabiki wengi zaidi.