YANGA AKILI ZAO ZIMEHAMIA HUKU SASA

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Yanga akili zao kwa sasa ni kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Mashujaa unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Lake Tanganyika, mwisho wa reli Kigoma.

Yanga inaongoza ligi ikiwa na pointi 52 baada ya kucheza mechi 20 ambazo ni dakika 1,800 kinara wa utupiaji mabao ni Clement Mzize mwenye mabao 10 ndani ya msimu wa 2024/25 na bao lake la 10 alifunga kwenye mchezo wa ligi dhdi ya Singida Black Stars ilikuwa dakika ya 13 akiwa ndani ya 18.

Kwenye mchezo huo Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 ambapo bao lingine lilifungwa na Prince Dube dakika ya 43 kwa pigo la kichwa akiwa ndani ya 18 na bao la Singida Black Stars lilipachikwa kimiani na Jonathn Sowah dakika ya 90 akimtungua kipa namba moja wa Yanga, Djigui Diarra.

Ali Kamwe, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa wanatambua ushindani ni mkubwa kwa sasa wanaendelea na maandalizi kwa ajili ya mchezo wao ujao unaotarajiwa kuchezwa Februari 23 2025.

“Tunafanya maandalizi ya mwisho kwa ajili ya mchezo wetu ujao ambapo tunatarajia kuondoka Dar Februari 21 siku ya Ijumaa kufanya maandalizi ya mwisho Kigoma, tunaamini mchezo utakuwa mgumu lakini akili zetu ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu kwenye mchezo wetu ujao.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.