MSHAMBULIAJI HUYU YANGA KWENYE ANGA ZA WAARABU

MKALI wa kucheka na nyavu ndani ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo ni ligi namba nne kwa ubora, Clement Mzize anatajwa kuwa kwenye rada za Waarabu wa Moroco ambao wanahitaji saini yake.

Ni Wydad Casablanca matajiri hawa wanatajwa kufika kwa mabosi wa Yanga na kuweka ofa yao mezani kwa ajili ya kupata saini ya kijana huyo ambaye ni mkali wa kucheka na nyavu na kutengeneza pasi za mabao akiwa ndani ya uwanja.

Kwenye mabao 50 yaliyofungwa na Yanga ndani ya ligi kahusika kwenye mabao 14, akifunga mabao 10 na kutoa pasi nne za mabao, Mzize alihusika kwenye penati dhidi ya KMC kwenye mchezo wa ligi uliochezwa Uwanja wa KMC Complex hivyo ni miongoni mwa wachezaji ambao wakiwa ndani ya uwanja wanajituma kutimiza majukumu yake.

Taarifa zinaeleza kuwa mabosi wa Wydad wanahitaji saini ya mshambuliaji huyo namba moja ndani ya kikosi cha Yanga akiwa anaongoza chati ya watupiaji ndani ya ligi namba nne kwa ubora akiwa katupia mabao 10 kibindoni na bao lake la 10 alifunga kwenye mchezo dhidi ya Singida Black Stars.

Ali Kamwe Ofisa Habari wa Yanga hivi karibuni aliweka wazi kuwa kuna ofa nyingi ambazo zipo kutoka sehemu mbalimbali zikihitaji saini za wachezaji wa timu hiyo hivyo mipango ikiwa sawa kila kitu kitakuwa wazi.

“Kuna ofa za wachezaji wengi ambao wanacheza ndani ya kikosi cha Yanga ikiwa ni pamoja na Mzize lakini kwa sasa bado yupo ndani ya Yanga ukifika wakati kila kitu kitakuwa wazi mashabiki msiwe na wasiwasi.”

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.