KOCHA Mkuu wa Namungo, Juma Mgunda ameweka wazi kuwa kilichowavuruga kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba uliochezwa Uwanja wa Majaliwa, Februari 19 2025.
Ni Derric Mukombozi nyota wa Namungo alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 32 hali iliyopelekea wacheze dakika 58 wakiwa pungufu mbele ya kikosi cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Fadlu Davids.
Baada ya dakika 90 ubao wa ulisoma Namungo 0-3 Simba, mabao ya Jean Ahoua ambaye alifunga mawili yote kwa mikwaju ya penati dakika ya 45 na 71 huku bao moja likifungwa na Steven Mukwala dakika ya 90.
Kwenye mchezo huo Simba ilipata penati tatu, mbili zilisababishwa na Shomari Kapombe na mpigaji alikuwa ni Ahoua na moja ilisababishwa na Elie Mpanzu mpigaji alikuwa ni Leonel Ateba dakika ya 51 mikono ya kipa Jonathan Nahimana iliokoa penati hiyo.
Mgunda amebainisha kuwa anaheshimu maamuzi ya mpiga filimbi akiwa uwanjani haijalishi anajua ama hajui lakini kilichovuruga mipango ya mchezo ule ni kadi nyekundu ambayo waliipata.
“Kusema ukweli ambacho kilivuruga mipango ya mchezo wetu ni kadi nyekundu ambayo mchezaji wetu alipata, unaona kwamba tulianza mchezo vizuri na mchezaji wetu muhimu ambaye alikuwa kwenye mpango kazi alionyeshwa kadi nyekundu hapo ndipo ambapo mambo yakabadilika.
“Tumepoteza mchezo wetu tunakubali kwa kuwa ikiwa unacheza na timu yenye wachezaji mkubwa kama Simba halafu mchezaji wako anapata kadi nyekundu mnakuwa wachezaji pungufu hapo inahitajika kazi kubwa. Siwezi kumlaumu mpiga filimbi iwe anajua ama hajui ninaheshimu maamuzi yao.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.