Kiungo wa klabu ya Yanga, Azizi Ki, ameendelea na mazoezi pamoja na wachezaji wenzake leo, kabla ya kuungana na mke wake, Hamisa Mobeto, kwa sherehe yao ya mapokezi (reception).
Sherehe hiyo inatarajiwa kufanyika baadaye leo katika Ukumbi wa Super Dome, Masaki, ambapo ndugu, marafiki, na mastaa mbalimbali wanatarajiwa kuhudhuria kusherehekea siku yao maalum.