Kamati ya uendeshaji na usimamizi wa Ligi imewapeleka kwenye kamati ya maadili ya shirikisho la mpira wa miguu nchini (TFF), ofisa habari wa klabu ya Yanga Ali Kamwe na Ofisa habari wa klabu ya Kagera Sugar, Hamis Mazanzala kwa tuhuma za kutenda makosa ya kimaadili kupitia machapisho yao kwenye kurasa za mtandao wa kijamii wa Instagram.
Taarifa ya kamati hiyo iliyokutana katika kikao chake cha Februari 12, 2025 imeeleza kuwa, viongozi na maofisa wa klabu wanazuiliwa kwa mujibu wa kanuni kutoa maandiko au matamshi chonganishi ama yanayoweza kuchafua taswira ya Ligi na mpira wa miguu kwa ujumla.
Wakati huo huo Bodi ya Ligi imewakumbusha maofisa habari/wasemaji wa klabu zote kuzingatia kanuni za Ligi na za maadili wakati wote wanapotekeleza majukumu yao, ili kuepuka kutoa kauli ambazo zinaweza kuzua chuki, taharuki au kuchochoea vurugu viwanjani.