ALI Kamwe ambaye Ofisa Habari wa Yanga amepelekwa Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, (TFF) na Ofisa Habari wa Kagera Sugar, Hamis Masanzala.
Taarifa iliyotolewa na Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania, (TPLB), imeeleza kuwa katika kikoa cha Februari 12 2025 walipitia mwenendo wa matukio ya ligi na kutoa angalizo kwa timu kutoruhusu mashabiki kuingia uwanjani wakati wa mechi ikitokea uwanja utafungwa.
Hiyo imetokana na mechi namba 139 Pamba Jiji 1-0 Azam FC, Klabu ya Pamba Jiji kutozwa faini ya milioni mbili kwa kosa la mashabiki wake kuvamia eneo la kuchezea mara baada ya mchezo kumalizika.
Kitendo cha mashabiki hao kuingia kiwanjani kilisababisha kuvunjika mahojiano ya makocha yaliyokuwa yakifanywa na mdhamini mwenye haki ya matangazo ya runinga,Azam TV.
Kuhusu Kamwe na Masanza taarifa imeeleza: Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi imewapeleka kwenye Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Ofisa Habari wa Yanga Ali Kamwe na Ofisa Habari wa Kagera Sugar, Hamis Masanzala kwa tuhuma za kutenda makosa ya kimaadili kupitia machapisho yao kwenye kurasa za mitandao ya kijamii, Instagram.”
CHAMPIONSHIP
Mechi ya Kiluvya FC 1-0 African Sports Klabu ya Kiluvya ya Pwani na African Sports ya Tanga zimepewa onyo kwa kosa la kuchelewa kuwasili uwanjani kinyume cha matakwa ya kanuni ya 17:15. Kiluvya waliwasili saa 8:43 mchana na African Sports waliwasili saa 8:40 badala ya saa 8:30 mchana.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.