SIMBA YAISHUSHA YANGA NAMBA MOJA

IKIWA Uwanja wa KMC Complex Simba imepata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Tanzania Prisons mchezo wa Ligi Kuu Bara ikiwa ni mzunguko wa pili.

Ukurasa wa mabao kwa Simba ulifunguliwa na Jean Ahoua dakika ya 29 anafikisha mabao 8 ndani ya ligi na bao la pili lilifungwa na Ellie Mpanzu dakika ya 44 likiwa ni bao lake la kwanza ndani ya ligi.

Ladack Chasambi mtoto wa maajabu amefunga bao moja dakika ya 46 akitumia pasi ya Shomari Kapombe ambaye alitoa pasi pia kwa Jean Ahoua.

Ateba ambaye alikosa nafasi za wazi zaidi ya nne alitoa pasi ya bao kwa Mpanzu ambaye alimtungua kipa Sebusebu aliyekuwa imara kwa kuokoa hatari zaidi ya sita za Simba.

Ni pointi 47 Simba wanafikisha wakiwa namba moja huku nafasi ya pili ikiwa mikononi mwa Yanga yenye pointi 46 zote zimecheza mechi 18 ndani ya ligi ambayo ushindani wake ni mkubwa kwa kila timu kupambania kupata pointi tatu.

Kapombe ambaye amehusika kwenye mabao mawili kati ya matatu ambayo yalifungwa na Simba yote kipindi cha pili amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.

 

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.