MCHEZO WA MNYAMA DHIDI YA DODOMA JIJI KUPANGIWA TAREHE

MCHEZO wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Dodoma Jiji uliotarajiwa kufanyika Uwanja wa KMC Complex Februari 15 2025 umeahirishwa hivyo utapangiwa taraehe nyingine.

Dodoma Jiji ilitoka kucheza mchezo wake wa ligi dhidi ya Namungo ugenini kwenye msako wa pointi tatu ambapo walitoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2 wakigawana pointi mojamoja. Februari 10 2025 saa 4 asubuhi gari lilipata ajali kwa kupinduka na kutumbukia mtoni.

Taarifa kutoka Dodoma Jiji imeeleza kuwa majeraha kwa sasa wanaendelea vizuri huku wakiendelea kupata matibabu ili warejee kwenye ubora zaidi.

Taarifa rasmi kutoka Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Bara, (TPLB) imeeleza kuwa sababu ya kuahirisha mchezo huo ni baadhi ya wachezaji na maofisa wa Dodoma Jiji kutokuwa katika hali nzuri kiafya baada ya basi la klabu walilokuwa wakisafiria kutoka Ruangwa mkoani Lindi kupata ajali.

 

Ajali hiyo imesababisha athari kwa Dodoma Jiji kwa kuchelewa safari kufika Dar pamoja na kuathiri maandalizi ya kiufundi kwa kuwakosa wachezaji na maofisa ambao walipata majeraha. TPLB itatangaza tarehe mpya hivi karibuni.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.