KIKOSI cha Dodoma Jiji kimepata ajali ya basi wakati wakirejea Dar kutoka Ruangwa walipomaliza mchezo wa ligi dhidi ya Namungo FC waliotoshana nguvu kwa kufungana mabao 2-2.
Kwenye mchezo huo Dodoma Jiji waligawana pointi mojamoja ugenini katika mchezo uliokuwa na ushindani mkubwa huku mlinda mlango Ngelekea Katembua akichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo.
Taarifa zimeeleza kuwa ajali hiyo imetokea katikati ya Nangurukuru na Somanga ambapo mpaka sasa jitihada za uokozi zinaendelea na haijaripotiwa taarifa ya kifo.
Taarifa zinaeleza kuwa basi lilipinduka na wachezaji wengi wamepata majeraha kwa timu hiyo ambayo ilikuwa inaelekea Dar kwa mchezo wa ligi dhidi ya Simba uliotarajiwa kuchezwa Februari 15.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.