JKT TANZANIA YAIBANA YANGA VINARA WA LIGI KUU BARA

WAJEDA JKT Tanzania wamevuna pointi moja mbele ya Yanga ambao ni vinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara wakiwa na pointi 46 baada ya kucheza mechi 18 msimu wa 2024/25 kutoka ligi namba nne kwa ubora.

Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu wa Yanga, Miloud Hamdi akiwa ugenini baada ya kuchukua mikoba ya Sead Ramovic ambaye alifikia makubaliano ya kuvunja mkataba na Yanga.
Inakuwa ni sare ya kwanza kwa Yanga baada ya kucheza mechi 18 ambapo ni ushindi katika mechi 15 na ilipoteza mechi mbili kwenye ushindani.
Pongezi kwa Wilson Nangu beki wa JKT Tanzania alikuwa anakaba kila hatari za Yanga na amechaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo uliochezwa Uwanja wa Isahmuyo.
Jitihada za Clement Mzize mshambuliaji namba moja kwa utupiaji ndani ya ligi akiwa na mabao 9 zilikwama kuipa matokeo Yanga, miongoni mwa majaribio aliyofanya Mzize ni dakika ya 38 na 45.
Kipa wa JKT Tanzania Yakub Suleiman alikuwa akipoteza muda mara nyingi kila akidaka mpira liha ya kutimiza majukumu yake akiwa kazini.
Miongoni mwa faulo za hovyo ambazo zimefanywa ni pamoja na ile ya Nassoro ilikuwa dakika ya 68 kwa Mudathir Yahya ambayo inaonekana ilikuwa ni kulipa kisasi cha faulo aliyochezea na Mudathir  dakika ya 33 jambo ambalo sio la kiungwana.

Kwa kosa hilo Nassoro alionyeshwa kadi ya njano na mwamuzi Ahmed Arajiga kwa kuwa mchezaji hakuwa na mpira katika eneo alilokuwa.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.