CLEMENT Mzize ni mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Yanga katika eneo la utupiaji akiwa amefunga jumla ya mabao 9 kati ya 42 yaliyofungwa na timu hiyo.
Mzize anaongoza chati ya watupiaji kwa idadi hiyo akifuatiwa na Elvis Rupia wa Singida Black Stars mwenye mabao 8 kama Ateba wa Simba.
Katika mabao 9 Mzize hajafunga kwa penalti kwa sanabu hakupewa majukumu hayo kwani Yanga ilipata jumla ya penalti 5 mpigaji Aziz Ki aliyepiga nne na Pacome aliyepiga moja.
Ipo wazi kwamba Mzize ndani ya msimu wa 2024/25 ndani ya kikosi cha Yanga ni mshambuliaji wa kwanza kufunga bao alifanya hivyo kwenye mchezo dhidi ya Kagera Sugar uliochezwa Uwanja wa Kaitaba.
Kwenye mchezo huo bao la kwanza lilifungwa na Maxi Nzengeli ambaye huyu ni kiungo mshambuliaji mwenye rekodi ya kuwa mfungaji wa bao la kwanza kwa wachezaji wote wa Yanga.
Mbele ya KenGold Mzize alifunga mabao mawili akifikisha idadi ya mabao 9 ambayo anayo kibindoni na pasi ambazo ametoa zikaleta mabao ni nne.
Yanga ni namba moja kwenye msimamo ikiwa na pointi 45 huku ikifuatiwa na Simba nafasi ya pili na pointi 44 zote zimecheza mechi 17 msimu wa 2024/25.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.