YANGA 6-1 KEN GOLD, UWANJA WA KMC

Ft: LIGI Kuu Bara

Yanga 6-1 Ken Gold

Mabao ya Yanga yamefungwa na: Prince Dube ametupia mabao mawili dakika ya 2, 45.

Clement Mzize mabao mawili dakika ya 6, 42

Pacome bao moja dakika ya 38

Duke Abuya dakika ya 85.

Suleman Rashid dakika ya 87

DAKIKA 45 mbele ya Ken Gold, Yanga inaongoza kwa mabao 4-0 ikiwa ni mchezo wa mzunguko wa pili kwa wababe hawa kukutana ndani ya msimu wa 2024/25.

Mabao ya Yanga yamefungwa na Prince Dube dakika ya 2 na bao la pili likifungwa na Clement Mzize dakika ya 6 akapachika bao la nne dakika ya 42 dakika ya 38 Pacome alipachika bao la tatu kwenye mchezo.

Pacome anafikisha mabao 7 ndani ya ligi akiwa ni miongoni mwa viungo wenye mabao mengi kwa msimu wa 2024/25 akiwa sawa na Jean Ahoua wa Simba.

Mzize anafikisha mabao 9 akiwa ni namba moja kwa utupiaji ikumbukwe kwamba kwenye mchezo uliopita dhidi ya Kagera Sugar alifunga bao moja ikiwa ni mchezo wa mwisho kwa Sead Ramovic ambaye kwa sasa hayupo ndani ya Yanga.

Ndani ya dakika 45 zinaonyesha kuwa Yanga imepiga mashuti 5 kuelekea lango la Ken Gold ambayo yamelenga lango huku Ken Gold ikiwa haijapiga shuti hata moja ambalo limelenga lango.

Ni mashuti mawili Yanga wamepiga yamekwenda nje ya lango huku Ken Gold wakipiga shuti moja ambalo limekwenda nje ya lango.

 

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.