RATIBA YA LIGI KUU BARA, SIMBA NA YANGA KAZINI

BURUDANI ya Ligi Kuu Tanzania Bara inayodhaminiwa na NBC inaendelea ambapo Februari 5 2025 kuna mechi kali mbili kwa wababe kuwa uwanjani kusaka pointi tatu muhimu na kivumbi kitaendelea Fenbruari 6 2025.

Tabora United v Namungo na Yanga itakuwa dhidi ya Ken Gold hizi mbili ni mechi za Februari 5 2025 kwa wababe kuwa kazini ndani ya ligi kusaka ushindi.

 FEBRUARI 6 2025

Tanzania Prisons v Mashujaa inatarajiwa kuchezwa saa 8:00 mchana, Uwanja wa Sokoine.

Dodoma Jiji v Pamba Jiji inatarajiwa kuchezwa saa 8:00 mchana, Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

Fountain Gate v Simba, Uwanja wa Tanzanite, Kwaraa, saa 10:15 jioni.

Azam FC v KMC, saa 1:00 usiku, Uwanja wa Azam Complex.

Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.