KOCHA bora Desemba mechi yake ya mwisho ilikuwa dhidi ya Kagera Sugar mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC, Complex.Katika mchezo huo baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 4-0 Kagera Sugar wakakomba pointi tatu muhimu na kukaa namba moja kwenye msimamo kwa saa 24.
Ni Sead Ramovic hatakuwa ndani ya kikosi cha Yanga baada ya kufunga pazia lake rasmi Februari Mosi akiwa na kikosi cha Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Ramovic alitwaa tuzo ya kocha bora Desemba 2024 amefikia makubaliano ya kuvunja mkataba wa timu hiyo Februari 4 2025.
Inatajwa kuwa Ramovic amepata dili jipya CR Belouizdad ya Algeria kwa ajili ya changamoto mpya ambapo atakuwa huko kwa ajili ya kutimiza majukumu yake.
Februari 4 alikuwa kwenye mkutano Waandishi wa Habari ikiwa ni kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ken Gold unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa KMC, Complex saa 10:00 jioni ambapo.Kocha huyo alibeba mikoba ya Miguel Gamondi ambaye alikutana na Thank You ndani ya kikosi cha Yanga aligotea nafasi ya tatu kwenye hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika.
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.