VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara Simba chini ya Kocha Mkuu, Fadlu Davids wamebainisha kuwa mchezo wao dhidi ya Tabora United hautakuwa mwepesi ila wamejipanga kuwakabili kwa mbinu uwanjani kwa kujituma mwanzo mwisho ndani ya uwanja.
Simba ni namba moja kwenye msimamo wa ligi namba nne kwa ubora ni pointi 40 zipo kibindoni baada ya mechi 15 ambazo wamcheza, huu ni mchezo wa mzunguko wa pili dhidi ya Tabora United ambapo kwenye mchezo wa kwanza walivuna pointi tatu, Uwanja wa KMC, Complex.
Simba iligawana pointi mojamoja na Coastal Union ya Tanga kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa KMC Complex baada ya dakika 90 ubao ulisoma Simba 2-2 Coastal Union kituo kinachofuata kwenye ligi ni ugenini dhidi ya Tabora United.
Ipo wazi kwamba Tabora United ilipata ushindi kwenye mechi za wababe wawili walio ndani ya tatu bora, Yanga 1-3 Tabora United na Tabora United 2-1 Azam FC.
Awesu amesema kuwa wanatambua mchezo huo ni muhimu hivyo wanaingia kwa tahadhari wakiwaheshimu wapinzani wao hao ambao wamekuwa wakipata matokeo kwenye mechi kubwa.
“Kila mchezo kwetu ni muhimu hasa ukizingatia kwamba wapinzani wetu watakuwa nyumbani na hii ligi ina ushindani mkubwa hivyo nasi tutaingia kwa tahadhari kupambana kuona namna gani tutapata matokeo mazuri uwanjani kwa kucheza kwa ushirikiano mkubwa.
“Ni mchezo ambao kila mchezaji yupo tayari na tutacheza kama fainali mchezo wetu kikubwa ni kuona kwamba tunapata pointi tatu muhimu uwanjani.”
Imeandikwa na Lunyamadzo Mlyuka, Mtunzi kitabu cha Ganzi ya Maumivu Kwenye Upendo, kukipata TUNAOMBA ODA 0756 028 371. Ni simulizi inayozungumzia maisha ya Kiafrika, usaliti, visa, furaha. Wakazi wa Njombe kitabu kinapatikana Mtaa wa Mpechi kwa Chris Jabari, Kigamboni kwa Tupokigwe, Posta karibu na Mnara wa Askari ukiwa unaelekea chuo cha IFM.