Home Sports HIVI NDIVYO MPANGO KAZI WA GAMONDI KIMATAIFA

HIVI NDIVYO MPANGO KAZI WA GAMONDI KIMATAIFA

UPO uwezekano mkubwa wa kiungo mshambuliaji mpya wa Yanga, Muivory Coast Pacome Zouzoua kuanza katika kikosi cha timu hiyo, kitakachovaana dhidi ya ASAS FC ya
nchini Djibouti.

Yanga itavaana dhidi ya ASAS katika mchezo wa hatua ya Awali ya Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa leo Agosti 20 Jumapili kwenye Uwanja wa Azam Complex, Mbagala
Jijini Dar es Salaam.

Pacome kwa michezo miwili ya mashindano waliyocheza Yanga ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam FC na Simba alianzishwa benchi na Kocha Mkuu wa timu hiyo, Miguel
Gamondi.

Kwenye mazoezi ambayo Yanga imefanya AVIC Town imekuwa na nyota wake wote ikiwa ni pamoja na Aziz KI, Mudathir Yahya, Djigui Diarra.

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa wachezaji wao wapya wakimataifa walioanzia benchi katika michezo iliyopita akiwemo Pacome, Hafidh
Konikon wapo fiti na tayari kuanza kucheza michezo ijayo ikiwemo dhidi ya ASAS.

Kamwe amesema kuwa kilichokabakia ni suala la kocha Gamondi kuwapa nafasi ya kumwanzisha katika kikosi chake, baada ya kuwepo fiti kwa asilimia moja kucheza
mchezo huo.

 Aliongeza kuwa wamepanga kuutumia mchezo huo kutuma salamu Afrika na kuiambia Afrika, kwamba timu yao imerudi katika Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kupata ushindi wa kwanza mnono dhidi ya ASAS.

“Jumapili tumepanga kuitumia kutuma
salamu Afrika na kuiambia Afrika kuwa Yanga imerudi Ligi ya Mabingwa kwa ushindi mnono tutakapocheza dhidi ya ASAS.

“Kwani msimu uliopita tulicheza Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, na sasa tumekuja kivingine katika Ligi ya Mabingwa Afrika. Tunajivunia usajili mkubwa ambao tumeufanya wa wachezaji wakubwa wenye uzoefu wa
kucheza michuano hiyo.

“Wapo baadhi ya wachezaji wapya ambao tayari wameonyesha viwango vyao na kukubalika, sasa zamu ya wengine ambao bado hawajaonyesha ubora na hapo namzungumzia Konkoni na Pacome tuliowasajili kwa ajili
ya michuano hiyo,” amesema Kamwe.

Previous articleYANGA YAWEKA MTEGO CAF, KOCHA AMUONYA BALEKE SIMBA
Next articleMASTAA SIMBA WATATU MAJANGA