Home Sports HAPA NDIPO AZAM ITAANZIA KUFANYA KAZI

HAPA NDIPO AZAM ITAANZIA KUFANYA KAZI

UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa utafanya mchakato wa kuboresha benchi la ufundi kwa kuanza na kumleta kocha mpya wa makipa.

Azam FC imeshuhudia mabingwa wa msimu wa 2022/23 kwenye ligi wakiwa ni Yanga chini ya Kocha Mkuu Nasreddine Nabi.

Kwenye mechi ambazo walikutana na Yanga ndani ya ligi walipata sare moja na kupoteza mchezo mmoja wa mzunguko wa pili.

Ipo wazi kuwa kwa msimu wa 2023/24 Dani Cadena aliyekuwa kocha wa makipa ambaye ameamua kutokuwa sehemu ya timu hiyo.

Pia Kali Ongala ambaye alikiongoza kikosi hicho kwenye mchezo wa mwisho dhidi ya Yanga ambao ulikuwa ni fainali ya FA naye pia hatakuwa kwenye kikosi hicho.

Katika taarifa aliyotoa Cadena kuhusu kuondoka kwake amewashukuru viongozi pamoja na  wachezaji aliokuwa akiwafundisha ikiwa ni pamoja na Wilbol Maseke, Idrisu Abdulai, Ali Ahamada.

Kocha huyo alikuwa sehemu ya kikosi kilichoshinda mshindi wa pili Azam Sports Federation kwa kufungwa 0-1 Yanga, Uwanja wa Mkwakwani.

Ofisa Habari wa Azam FC, Hasheem Ibwe amesema kuwa watafanya maboresho kwenye kila idara ambayo itakuwa inahitajika.

“Azam FC ni timu kubwa na tunafanya kazi kikubwa katika kazi zetu zote hivyo kwenye sekta ya uboreshaji kikosi tutafanyia kazi kila sehemu ambayo itakuwa na uhitaji,” amesema Ibwe.

Previous articleYANGA SC:KOCHA ANAYEKUJA ATATIKISA NCHI, FAGIO LAPITA SIMBA
Next articleTAIFA STARS KAZI INAENDELEA