Home Sports MFARANSA WA AZAM FC ANASUKA KIKOSI KAZI KIMATAIFA

MFARANSA WA AZAM FC ANASUKA KIKOSI KAZI KIMATAIFA

DENIS Jean, Kocha Mkuu wa Azam FC raia wa Ufaransa amesema kuwa kwa sasa mpango kazi uliopo ni kuandaa utimamu wa kikosi hicho kuelekea kwenye mechi za kimataifa pamoja na ligi.

Kocha huyo ambaye amesaini dili la mwaka mmoja kuchukua mikoba ya Abdi Hamid Moallin mchezo wake wa kwanza wa ligi alishuhudia timu hiyo ikishinda bao 1-0 dhidi ya Mbeya City, Uwanja wa Sokoine.

Mfaransa huyo amesema: “Tuna muda mrefu ambao tutakaa kutokana na kutokuwa na mechi jambo ambalo tunafanya kwa sasa ni kufanya maandalizi na kucheza mechi za kirafiki ambazo zitatufanya tuwe imara.

“Tunahitaji kuwa na kikosi imara kwenye mechi zetu za kitaifa na kimataifa nina amini kwenye uwezo wa wachezaji wetu na wanazidi kuonyesha juhudi kwenye kazi,”.

Mchezo ujao wa Azam FC ni dhidi ya Tanzania Prisons unatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Septemba 30.

Septemba 23, Azam FC ilicheza mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya TP Mazembe na zilitoshana nguvu kwa kufungana bao 1-1.

Tayari kikosi kimerejea Dar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons.

Previous articleSIMBA WAFUNGUKIA AUSSEMS KUREJEA
Next articleMGUNDA AJILIPUA SIMBA, NABI AWAINGIZA CHAKA WASUDAN