Home Sports MKUDE:HAIKUWA RAHISI KUSHINDA

MKUDE:HAIKUWA RAHISI KUSHINDA

JONAS Mkude, kiungo wa Simba amesema uwa haikuwa kazi rahisi kushinda mbele ya Tanzania Prisons kutokana na ugumu wa timu hiyo.

Mkude alipachika bao la ushindi kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, dakika ya 85 kwa pasi ya Kibu Dennis.

“Kucheza na Tanzania Prisons kunahitaji kujipanga na timu ambayo itapata nafasi inaweza kushinda hivyo tulifanya maandalizi mazuri na tulipambana kusaka ushindi,” amesema.

Ni bao la kwanza la Mkude kwenye ligi msimu wa 2022/23 akiwa na uzi wa Simba.

Pia ni mchezo wa kwanza kwa Kocha Mkuu, Juma Mgunda kushuhudia wakipata pointi tatu kwenye mchezo wa ligi.

Previous articleFEDHA INAONGEA, YANGA WANAISHI KISHUA, MGUNDA APEWA SIKU 180
Next articleODDS KUBWA GEMU ZA UCL NA EFL KUTOKA MERIDIANBET KUELEKEA WIKENDI!