Home Sports NABI AFICHUA SABABU YA KUTOFUNGWA DK 3,600

NABI AFICHUA SABABU YA KUTOFUNGWA DK 3,600

NASREDDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amefichua kuwa kutopoteza kwenye mechi za ligi kwa muda mrefu kunatokana na jitihada za wachezaji kusaka ushindi.

Ni mechi 40 za ligi Nabi kaongoza bila kuonja ladha ya kupoteza mchezo ikiwa ni dakika 3,600 zimeyeyuka.

 Aprili 25,2021 ilikuwa ni mara ya mwisho Yanga kufungwa ilipoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Azam FC uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Nabi amesema kuwa sio kitu rahisi kucheza mechi nyingi bila kufungwa na inahitaji juhudi zaidi kwa wachezaji kupata matokeo.

“Unaona kwamba msimu huu ligi ni ngumu na kilamechi tunatambua kwamba itakuwa na ushindani mkubwa, sio rahisi kushinda mechi zote na ili tusifungwe ni lazima tuongeza juhudi.

“Wachezaji nimewaambia kwamba kazi yetu moja ni kutafuta ushindi kwenye mechi zote bila kujali tunacheza na timu ipi, mfano mchezo wetu dhidi ya Azam kabla hatujacheza nao nilijua utakuwa mgumu.

“Kuwaangalia wapinzani wakiwa wanacheza haina maana kwamba inaweza kukupa matokeo unayotaka kwenye mechi zako,” alisema Nabi.

Previous articleRATIBA ZA MECHI KUBADILISHWA ENGLAND
Next articleGEITA NDANI YA SUDAN, MPOLE ABAKI DAR