
MABINGWA WATETEZI WA KOMBE LA EURO 2024, ITALIA WATOLEWA
Mabingwa watetezi wa kombe la Mataifa Ulaya EURO 2024, Italia wamesukumizwa nje ya michuano hiyo kufuatia kipigo cha 2-0 dhidi ya Uswisi kwenye hatua ya 16. Mabao la Remo Freuler (dk ya 37) na Ruben Vargas 46’ yameipeleka Uswisi robo fainali ya michuano hiyo.