>

YANGA, SIMBA MZIGONI LEO LIGI KUU

LIGI Kuu ya kabumbu Tanzania bara inaendelea tena leo Septemba 29 kwa mechi nne kwenye viwanja mbalimbali ambapo Mnyama, Simba Sc akiwa ugenini kwenye mashamba ya mizabibu wakiikabili Dodoma Jiji Fc.

Mchezo huo wa raundi ya nne wa Ligi hiyo utapigwa katika dimba la Jamhuri Dodoma mishale ya saa 12:30 jioni huku Mnyama akiangazia kuendelea rekodi ya ushindi kwa asilimia 100 baada ya ushindi wa mechi tatu mfululizo bila kuruhusu bao.

Rekodi zinambeba Mnyama pale wawili hawa wanapokutana kwenye NBC Premier League akishinda mara zote dhidi ya Wakulima hao wa zabibu kuanzia msimu wa 2020/21.

Msimu wa 2020/21
Dodoma 1-2 Simba
Simba 3-1 Dodoma Jiji

Msimu wa 2021/22
Dodoma 0-1 Simba
Simba 2-0 Dodoma

Msimu wa 2022/23
Simba 3-0 Dodoma
Dodoma 0-1 Simba

Msimu wa 2023/24
Simba 2-0 Dodoma
Dodoma 0-1 Simba

Leo Septemba 29, 2024

DODOMA JIJI FC 🆚️ SIMBA SC
🏟️ Jamhuri, Dodoma
⏰ 12:30 jioni

MECHI ZINGINE LEO NBCPL

14:00 SINGIDA BLACK STARS 🆚️ JKT TANZANIA
🏟️ CCM, Liti

16:00 Mashujaa 🆚️ Azam FC
🏟 Lake Tanganyika

21:00 Yanga SC 🆚️ KMC Complex
⏰️ 21:00
🏟 Azam Complex