Jamaa wapo serious sana na ligi ya msimu huu. Yaani wanaenda nayo hatua kwa hatua kuhakikisha kuwa hawaachi alama yoyote ile.
Michezo minne, ushindi kwenye michezo yote. Alama 12 mpaka sasa na baridi ikiendelea kuwapiga pale kileleni mwa msimamo. Hao ni SINGIDA BLACK STARS.
Wamemchapa Pamba Jiji leo pale pale CCM Kirumba bao moja kwa sifuri. Mkifanya masikhara mtawakuta wanapiga parade la ubingwa.
Alianza Kennedy na Manyama halafu mhuni Tra Bi yupo benchi. Joseph Guede yupo benchi na Rupia anakiwasha. Yahya Mbegu ametulia tu kwenye mbao ndefu na Ibrahim Imoro anauiga ndani. Ayoub Lyanga yupo benchi lakini ndani kandanda linapigwa vizuri tu. Hawa jamaa wamedhamiria msimu huu.
FT: Pamba Jiji 0-1 Singida Black Stars
⚽ Emmanuel Keyekeh