>

UGANDA, ‘THE CRANES’ YAPATA USHINDI WAKE WA KWANZA KWENYE MICHUANO YA KUWANIA KUFUZU AFCON 2025

TIMU ya Taifa ya Uganda, ‘The Cranes’ imepata ushindi wake wa kwanza kwenye michuano ya kuwania kufuzu AFCON 2025 kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya Congo katika dimba la Nelson Mandela National (Kampala).

FT: Uganda 🇺🇬 2-0 🇨🇬 Congo
⚽ Kayondo 21’
⚽ Ssemugabi 86’

The Cranes wapo kileleni mwa msimamo wa kundi K alama 4 baada ya mechi mbili.

Katika mchezo mwingine timu ya taifa ya Ghana imelazimishwa sare ya 1-1 dhidi ya Niger kwenye mchezo wa Kundi F

FT: Niger 🇳🇪 1-1 🇬🇭 Ghana
⚽ Sako 81’
⚽ Seidu 44’